July 14, 2018



Kiungo mkongwe nchini Mrisho Ngassa amerejea Yanga rasmi na kukabishiwa jezi mbele ya wanahabari.

Ngassa amerejea na kujiunga na Yanga tena baada ya safari yake ndefu ndani na nje ya nchi.

Kiungo huyo mtoto wa kiungo wa zamani wa Simba, Khalfan Ngassa, aliondoka Yanga na kwenda Afrika Kusini alipojiunga na klabu ya Free State Stars, lakini hakudumu aliporejea nchini na kujiunga na Mbeya City.

Baada ya Mbeya City alihamia Ndanda FC baada ya mpango wake wa kurejea Yanga kushindikana lakini kwa ajili ya msimu ujao, inaonekana mambo ni safi kwake.

3 COMMENTS:

  1. Duh Peter Manyika nae lini atasajiliwa

    ReplyDelete
  2. Peter Tino mshambuliajj qa zamani wa Pan Africans na yeye keshasajiliwa Yanga. Kweli Yanga tuko makini sana na usiku wetu wa kimya kimya. Yanga hoyeeee

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndiyo Yanga bhana. Hata Boban nae ndani ya nyumba. Watatukoma sana safari hii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic