July 29, 2018


Juventus wanaamini kiungo wa kati Paul Pogba yuko tayari kurejea kwenye klabu hiyo ya nchini Italia, na wako tayari kumuuza mshambuliaji Gonzalo Higuain, 30,kiungo wa kati Miralem Pjanic na walinzi Daniele Rugani, 24, and Mattia Caldara, 24, ili kumgharamia mchezaji huyo mwenye miaka 25. (Sunday Mirror)

Real Madrid inaelekea kuachana na mpango wake wa kumsaini Eden Hazard kutoka Chelsea baada ya kukataa bei ya paundi mil 200 aliyowekewa mchezaji huyo.(Sunday Express)

Chelsea iko tayari kumnyakua kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, kwa kitita cha pauni milioni 30.Aaron amebakisha mwaka mmoja kumaliza mkataba wake na washika bunduki hao. (Mail on Sunday)

Manchester United inapanga kumnyakua mlinzi wa Barcelona Yerry Mina,23. (Sun on Sunday)

Borussia Dortmund wanajiandaa kumuuza Christian Pulisic msimu huu kwa gharama ya pauni milioni 65, Chelsea na Liverpool ni miongoni 'mwa timu zilizoonyesha nia ya kumchukua.(Mail on Sunday)

liverpool inataka kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, kwa pauni milioni 26, lakini Watford wanamtaka mchezaji huyo kwa mkopo

Westham inajiandaa kumnyakua beki wa kati Domagoj Vida kutoka Besiktas, Monaco nao wakionyesha nia ya kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka 29(Fanatik, via Sunday Express)

Meneja wa Burnley Sean Dyche anataka kumsajili mshambuliaji wa Stoke City,Peter Crouch, 37, kwa dili la pauni 500,000.(Sun on Sunday)

Everton wamekubali dau la hadi paundi 25 kwa Barcelona Kwa ajili ya Beki Lucas Digne (25 ) raia wa Ufaransa. (Goal.com)

Arsenal inamlenga Steven Nzonzi, 29, kiungo wa kati wa zamani wa Blackburn na Stoke ambaye sasa anakipiga Sevilla, yu mbioni kujiunga na Roma kwa kitita cha zaidi ya pauni milioni 29

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic