July 14, 2018


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za msiba wa aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Matagi Yasoda.

Katika salamu zake za rambirambi Rais wa TFF Ndugu Karia amesema mama Yasoda enzi za uhai wake alikuwa mwanamichezo mzuri hivyo aliyeshiriki katika shughuli mbalimbali za michezo hususani mpira wa Miguu.

“Kifo cha mama Yasoda kimenishtua nilimfahamu kama mwanamichezo mzuri katika ngazi ya uongozi aliyeshiriki kikamilifu katika michezo,kwa niaba ya TFF natoa pole kwa familia,ndugu,jamaa,marafiki na familia ya michezo” alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Juliana Yasoda alifariki juzi baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic