July 29, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika programu ya mazoezi nchini Uturuki kwa takribani wiki moja sasa, uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, umesema timu hiyo haitoshikika msimu ujao.

Simba ipo Instabul katika Milima ya Kartepe ikijifua kwa maandalizi ya tamasha la Simba Day ambalo khufanyika Agosti 8 kila mwaka pamoja na msimu mpya ujao wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zimeeleza Djuma amesema kila mchezaji ameahidi makubwa kuelekea pazia la ligi kufunguliwa ambapo Simba itaanza kucheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Aidha, Kocha huyo amefunguka na kusema uwepo wa Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems umechangia kwa wachezaji wote kujituma zaidi mazoezini ili kumuonesha uwezo walionao.

Mbali na programu za mazoezi, kikosi cha Simba kimekuwa kikiingia darasani kupewa mafunzo mbalimbali ili kuwaongezea uelewa wachezaji wake ikiwemo elimu ya saikolojia.

Baada ya kambi hiyo kumalizika, SImba wataanza kurejea jijini Dar es Salaam Agosti 4 tayari kwa maandalizi ya Simba Day na mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Suhar utakaopigwa Agosti 12 Uwanja wa CCM Kirumba.

3 COMMENTS:

  1. Safi sana. Ni vizuri kuwa na timu yenye ushindani wa namba hasa kwa wachezaji waelewa yakwamba ukupigao sio ukumizao bali ndio ukufunzao. Simba itanufaika sana na mchanganyiko wa maana wa wachezaji wao na ingekuwa raha sana kama viongozi na wachezaji wa timu nyengine zinazoshiriki ligi kuu bara kulichukulia suala la nyongezo la wachezaji wa kigeni kama nafasi hadimu ya kuinua ari ya wachezaji badala ya kulilia tu. Kama mchezaji anaogopa kushindana katika ardhi yake vipi akibahatika kupata changamoto katika ardhi ngeni?

    ReplyDelete
  2. Lakini Tambwe anakubezeni. Masikini roho yake kwasababu haijui hatma yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic