RAIS John Magufuli na mkewe Janeth, wamejumuika na watu mbalimbali kumpa pole Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, aliyefiwa na mama yake mzazi, Bi. Asteria Kahabi Kapela, alfajiri Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa.
Msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment