TAMBWE AFUNGUKA MAZITO KUHUSIANA NA YANGA
Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Championi, Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti.
“Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitegemea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata matokeo.
“Nadhani huu ni wakati wa kuendelea kushikamana, mashabiki wetu hawapaswi kuendelea kukata tamaa japokuwa hatupo katika wakati mzuri kama ilivyokuwa zamani, hakuna ambaye ana furaha na kinachotokea kwa sababu wote tunataka kufikia mafanikio na ukiangalia tunaelekea kwenye ligi kwa nini wakate tamaa,” alisema Tambwe.








Mmmmmhhhhhh haya bana
ReplyDeleteUragaanira neeza.Mambo ni magumu sana
ReplyDeleteHivi kweli ndugu mwandishi hayo aliyosrma Tambwe ndiyo mazito?Au unatuona hatujui nini maana ya maneno mazito? Ukweli ni kwamba hakuna jipya aliloongea
ReplyDeleteHuuu alikosea chupuchupu kutemwa lakini yanga ilipoishiwa ndio wakaona abakie angalau liwepo jina lake lakini msimu mzima hakuwa na mana na yanga walishindwa angalau kumpeleka India na kabaki kututumka ionekane yupi. Anacheza dakika kuki halafu anapumzishwa pamoja na mdogo wake Ajibu alieongoza katika migomo ya kudai hela
ReplyDeleteKwa hiyo!!!??
ReplyDeleteYanga imebaki jina tuu kwa sasa tunasubir mechi yao ya marudiano na gormahia wapigwe 6-0 ili watimiz idad yao waliyoizoea kufungwa, hao ndo Wa kimataifa wasindikizaj
ReplyDelete