July 26, 2018


Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya ku­fungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Championi, Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa maru­diano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti.

“Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitege­mea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata ma­tokeo.

“Nadhani huu ni wakati wa kuende­lea kushikamana, mashabiki wetu hawa­paswi kuendelea kukata tamaa japokuwa hatupo katika wakati mzuri kama ilivyokuwa za­mani, hakuna ambaye ana furaha na kinacho­tokea kwa sababu wote tunataka kufikia mafanikio na ukiangalia tunaelekea kwenye ligi kwa nini wakate tamaa,” alisema Tambwe.

6 COMMENTS:

  1. Uragaanira neeza.Mambo ni magumu sana

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli ndugu mwandishi hayo aliyosrma Tambwe ndiyo mazito?Au unatuona hatujui nini maana ya maneno mazito? Ukweli ni kwamba hakuna jipya aliloongea

    ReplyDelete
  3. Huuu alikosea chupuchupu kutemwa lakini yanga ilipoishiwa ndio wakaona abakie angalau liwepo jina lake lakini msimu mzima hakuwa na mana na yanga walishindwa angalau kumpeleka India na kabaki kututumka ionekane yupi. Anacheza dakika kuki halafu anapumzishwa pamoja na mdogo wake Ajibu alieongoza katika migomo ya kudai hela

    ReplyDelete
  4. Yanga imebaki jina tuu kwa sasa tunasubir mechi yao ya marudiano na gormahia wapigwe 6-0 ili watimiz idad yao waliyoizoea kufungwa, hao ndo Wa kimataifa wasindikizaj

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic