Mashindano ya Vijana nchini yanatarajiwa kufanyika kati ya Mwezi Oktoba 2018 – April 2019 kama ambavyo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alitangaza msimu huu kutawepo Mashindano ya Vijana kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 15,17 na 20.
Katika marekebisho ya Kanuni msimu wa 2018-2019 vilabu vyote vya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraa la Pili vinalazimika kuwa na timu za Vijana.
Timu za Ligi Kuu zinapaswa kuwa na timu za vijana chini ya miaka 20 (U-20) na chini ya miaka 17 (U-17), huku timu za Daraja la Kwanza na Daraja la Pili zikitakiwa kuwa na timu za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17).
Ligi ya U20 itaanza Oktoba ikishirika timu za vijana (U-20) kwa vilabu vyote kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, huku Mashindano ya U17 yatakyoshirikisha timu 68 za vijana kutoka vilabu vya Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili yakitarajiwa kuanza Novemba, 2018.
Michuano ya U15 itashirikisha jumla ya timu 35 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ambayo inatarajiwa kuchezwa mwezi Disemba, 2018.








Tunapenda kuiga lakini tunaishia kushindwa
ReplyDeleteFedha IPO(udhamini)?
ReplyDelete