July 26, 2018


Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umetoa kauli ya kushangaza kuhusiana na usajili wa wachezaji kabla ya dirisha kufungwa leo saa 6 usiku.

Msemaji wa timu hiyo, Thobias Kifaru, amesema wao hawana haraka kabisa ya kufanya usajili huo kwani mpaka kufikia saa 6 usiku ni masaa mengi kwao.

Kifaru ameeleza masaa hayo ni mengi sana kwao na akisema kuwa wao ni klabu kongwe hivyo hawana haraka ya kufanya usajili huo sababu bado muda unaruhusu.

"Kwani kuna haraka gani ya kusajili!! Mpaka kesho bado kuna masaa kibao yamesalia dirisha kufungwa, sisi ni klabu kongwe bwana tunafanya mambo kitaalamu, usiwe na wasiwasi juu ya hilo" alisema.

Kauli hiyo kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukumbushia kwa msisitizo kuwa klabu zote zinapaswa kukamilisha usajili wao haraka na baada ya tarehe saa 6 usiku wa leo hakutakuwa na nyongeza ya muda.


2 COMMENTS:

  1. kwani wazee wa kimya kimya tayari?????????

    ReplyDelete
  2. Tunaombeni matokeo ya SIMBA uturuki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic