TFF YAWAJIBU WALIOHOJI JUU YA ONGEZEKO LA WACHEZAJI KIMATAIFA
Na George Mganga
Baada ya hoja mbalimbali kutolewa na wadau wa soka nchini juu ya ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka 7 mpaka 10, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, amelitolea ufafanuzi leo.
Rais Karia amesema kuwa klabu ndizo zilipendekea kuwe na ongezeko hilo na mwisho wa siku aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga, alikubali ombi hilo kupitia kikao walichokaa Juni 30 2018.
Baada ya mapendekezo hayo kupitishwa kunako Bodi ya Ligi, baadaye Kamati ya Utendaji ya TFF ilikaa na kuyajadili kisha kufikia mwafaka wa omgezeko hilo kupitishwa.
Hatua ya Karia kutolea ufafanuzi huo ni kutokana na baadhi ya malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuanza kuhoji imekuwaje TFF imefikia uamuzi huo kuliko kujali vipaji vya wazawa kuvilinda.
Mapema baada ya ongezeko hilo kuwekwa hadharani, wengi walikuwa walifunguka na kueleza inaweza kuwa chanzo cha kuvunja ndoto za wazawa wengi kutoka kisoka baada ya idadi ya wageni kuwa wengi.








Hii ndo bongo...
ReplyDeleteHii ndo bongo...
ReplyDeleteHoja za ongezeko la wachezaji wa kigeni eti litaua vipaji vya wazawa hazina mashiko.Hivi wageni mnawaogopa kwani wana miguu minne?...wachezaji wazawa wanabidi wapate changamoto toka kwa wageni.Klabu zinaingia kwenye mfumo wa mabadiliko hivyo inahitaji matokeo ili ifanye biashara na wadhamini.Ningewaelewa Kama wageni watakatazwa kucheza ndondo sababu kule ndiko kwenye kutafuta vipaji au walau wasingeruhusu kusajili magolikipa Wageni.tusiwe waoga wa changamoto kwani mpira ni pesa
ReplyDelete