July 24, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiwa Uturuki kwa ajili ya kambi maalum ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, wachezaji wengine wanatarajiwa kukwea pipa kesho Jumatano.

Wachezaji hao ni Meddie Kagere aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC, Haruna Niyonzima na Erasto Nyoni ambao viza zao za kusafiria zilichelewa kukamilika.

Kuchelewa kwa viza zao kulisababisha washindwe kwenda na kikosi kilichosafiri Jumapili hivyo ikabidi wasalie nchini mpaka pale taratibu nzima za kuzikamilisha zitakapomalizika.

Kikosi hicho kipo Instabul kikijifua kwa maandalizi ya tamasha la Simba litakalofanyika Uwanja wa taifa, Dar Es Salaam, Agosti 8 2018 kama ilivyo ada.

Simba hufanya tamasha hilo maalum kuwatambulisha wachezaji wao watakaokuwepo kwenye kikosi cha msimu wa 2018/19.

3 COMMENTS:

  1. Hapo sawa maana vyombo vilikua vnataarifu kwamba wachezaji ambao hawapo na timu ni tisa tu na miongoni mwa Hawa aliyekua anatajwa ni Erasto tu ilihali wengine hawaonekani kambini (Kagere na Niyo)huku wengine wakitajwa kwamba hawakusafiri na timu ilihai kambini wanaonekana akiwemo Salamba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli, kuna mambo yanatuchanganya sana. Nilishangaa kuona picha za Adam Salamba akiwa Uturuki wakati vyombo mbalimbali viliripoti kuwa amebaki kwa kuwa yu majeruhi. Vipi kuhusu Ndemla ambaye ilisemekana amebaki kukamilisha mkataba mpya? Sijawahi kusoma popote orodha ya wachezaji wa Simba waliopo Uturuki. Halafu, je, timu imeshakamilisha usajili wake? Ningekuwa mwanahabari ningeuliza maswali haya.

      Delete
    2. kwani hujui majority ya wandishi wa habari ni Yanga.Ingekuwa ni Yanga wako Uturuki wangewapa kiki kiasi unaona kinyaa kusoma wangekueleza mpaka toilets wanazotumia.Sijui waandishi walikuwa wanalipwa enzi hizo ili waandike utumbo wao?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic