July 24, 2018


Kufuatia Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kuachia ngazi jana, baadhi ya wadau na wachama wa Yanga wengi wamepongeza uamuzi huo.

Wanachama hao wamekubaliana na maamuzi ya Sanga huku wengi wakieleza ni sahihi kwake kufanya hivyo kutokana na mwenendo mzima wa klabu ulivyo sasa.

Mbali na mwenendo wa klabu, wachama hao wamesema Sanga alikuwa amechelewa wakieleza alipaswa kufanya hivyo mapema ili kuwapa nafasi wengine.

Wengi wao wamefunguka na kueleza Sanga alikuwa haiendeshi Yanga kwa ueledi na kupelekea kuleta kutokuelewana baina yake na viongozi wengine haswa wa kamati ya utendaji waliojiuzulu akiwemo Khalfan Hamis.

Kitendo cha Sanga kuachia ngazi kimewakonga nyonyo wachama hao pamoja na baadhi ya mashabiki kwa maamuzi yake na sasa itabidi ikiwezekana uchaguzi ufanyike ili mbadala wa Mwenyekiti apatikane.

Sanga ameeleza sababu mojawapo iliyompelekea kuachia ngazi ni kushutumiwa na baadhi ya watu akisema walipanga wkwenda kuvamia kwake wakiwa na mapanga jambo ambalo ameona linaweza kuhatarisha maisha yake.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic