July 27, 2018


Hatimaye uongozi wa klabu ya Yanga umekata mzizi wa fitina kwa kumalizana na mchezaji wake, beki Kelvin Yondani kwa kusaini naye mkataba wa miaka miwili.

Hatua hiyo imefikiwa mwafaka mara baada ya mazungumzo mrefu baina ya uongozi na Yondani kumalizana vizuri.

Mkataba huo amesaini zikiwa zimesalia saa kadhaa dirisha la usajili nchini kufungwa wakati hapo awali alikuwa anatajwa kutua Simba.

Licha ya tetesi za beki huyo kuelezwa anawindwa na Simba, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara aliibuka na kukanusha vikali kauli hiyo akisema hakuna ukweli wowote juu ya Yondani kuhitajika Simba.

Beki huyo sasa atasalia Yanga mpaka mwaka 2020 baada ya kutia kandarasi hiyo ya miaka miwili kuendelea kukipiga na Yanga

1 COMMENTS:

  1. unahitaji utulivu sana katika kusoma mkataba, ukiwa umesimama si utulivu wa uhakika ni shinikizo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic