July 29, 2018


Yanga wamemwambia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ mziki wa Emmanuel Okwi na Meddie Kagere wa Simba hatauweza msimu huu badala yake ajiandae kisaikolojia kuwa meneja tu.

Hiyo inamaanishwa kwamba Hafidh Saleh ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 10 atapangiwa majukumu mengine kwenye benchi la ufundi.

Cannavaro akiwa nahodha wa timu hiyo amenyanyua makombe matano kati ya hayo matatu ya Ligi Kuu Bara, moja la Kagame na Ngao ya Jamii moja.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema wameamua kubadilisha benchi la ufundi kwa kumpa Cannavaro nafasi ya umeneja na Hafidhi atakuwa mratibu lengo ni kuboresha benchi la ufundi kwani awali kwenye michuano ya kimataifa walikuwa hawana mtu sahihi wa kufuatili vitu mbalimbali vya michuano ya kimataifa pindi walipokuwa wakishiriki.

Alisema baada ya kuona hivyp wakafikia muafaka kwamba Hafidhi apewe nafasi ya uratibu kwani anamudu kushughulikia ishu hizo ili kuepukana na adhabu ambazo zinaweza kutolewa na Shirikisho la Soka Afrika’Caf’.

Pia kocha wa makipa Juma Pondamali hatokuwa sehemu ya kikosi hicho kuanzia sasa na sasa wanatafuta mbadala wake mwenye uwezo zaidi.

“Tumeamua kuimarisha benchi la ufundi kwa kumpa umeneja Cannavaro na Hafidhi atakuwa mratibu wa timu, pia tumeachana na Pondamali ambapo sasa tunatafuta mbadala wake,” alisema Nyika.

Alipotafutwa Cannavaro kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Sipo Dar, hapa ninapoongea na wewe nipo Hospitali ya Mnazi Mmoja huku Unguja, Zanzibar nilipokuja leo (jana) kwa ajili ya kumuuguza mama yangu.

“Hivyo sitaweza kuzungumzia hilo kwa hivi sasa nivumilie nitakupigia tutaongea vizuri, mama yangu amepata ‘stroku’ mguuni na mkononi,” alisema Cannavaro.


CHANZO: CHAMPIONI

7 COMMENTS:

  1. KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii comment kila mara inarudiwa kwann ??Tumekuchoka kawaambie viongoz km unahis awaelew sawa .......

      Delete
  2. Au tumechoshwa na habari za kinafki alokwambia kastaaf kwa 7bu ya Okwi na Kagere nani mbona kwenye nukuu ya Huseni Nyika hatujayaona hayo maneno Acha unafki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiukweli hata mimi sijamuelewa mwandishi,ligi ina timu 20 na kila timu itacheza takribani michezo 38,sasa Kanavaro atawakimbiaje Okwi na Kagere atakaokutana nao kwenye gemu 2 tu za ligi?

      Uandishi wa kijuha unaharibu maana halisi ya Tasnia ya habari.

      Delete
    2. Mazingira yanaonyesha. Ushahidi wa mazingira

      Delete
  3. Mwandishi acha unafiki wapi kweny habar yako imeonesha Cannavaro kawaogopa Kagere na Okwi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic