August 13, 2018


Na George Mganga

Baada ya aliyekuwa beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro. kutangaza kustaafu soka, Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka na kumpa heshima yake mongwe huyo.

Manara ameeleza kuwa Cannavaro ni moja ya mabeki bora kuwahi kutokea katika taifa hili la Tanzania ndani ya miaka 10 iliyopita.

Manara ameshauri itakuwa vema kama Cannavaro akaagwa kwa mechi moja kupigwa Uwanja wa Taifa baina ya timu yake 'Friends Of Nadir' dhidi ya Yanga kutokana na mchango wake ndani ya soka la Tanzania.

Lakini licha ya kushauri hilo, Cannavaro aliagwa jana kwenye wa Jamhuri Morogoro kwa Yanga kukipiga na Mawenzi Merket ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Baada ya kustaafu, Cannavaro alikabidhi jezi yake yenye namba 23 kwa beki Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye atakuwa anaivaa kwa mechi zijazo akiwa na kikosi hicho.

3 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Ujinga haujawahi mwacha mtu salama hajapanga ametoa ushauri

      Delete
  2. Kabisa kwa mtu kama cannavaro inatakiwa iwe hvyo achague yeye mechi ya wakongwe wenzake aliowah kucheza nao ili awaage pia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic