August 13, 2018


Na George Mganga

Baada ya kukabidhiwa jezi namba 23 kutoka kwa Nadir Haroub 'Cannavaro', beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amefunguka machache juu ya kukabidhiwa uzi huo.

Ninja ameeleza kuwa anajisikia faraja zaidi kupata jezi hiyo kutoka kwa Cannavaro ambaye ameichezea Yanga kwa mafanikio makubwa pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya Mawenzi Market ambao ulikuwa maalum kwa kumuaga Cannavaro, Ninja ameahidi kuifanyia makubwa jezi hiyo kama ambavyo mhusika amehitaji.

"Kusema ukweli nimefarijika kupata jezi ambayo ina heshima kubwa Yanga kutokana na mchezaji mwenyewe, nitaipigania kuweza kuipa heshima kama ambavyo Cannavaro ameniagiza ndani ya Uwanja"




3 COMMENTS:

  1. Pambana Ninja waweza kuwa mrithi wa Canavaro kujituma na nidham nje na ndan ya uwanja ndo siri kubwa ya Nahodha mstaafu Canavaro kwel alikuwa mtu wa watu anastahir pongezi Asante Canavaro

    ReplyDelete
  2. Ukitambua, ukajituma Mungu akiweka kudra zake utafikia malengo.

    ReplyDelete
  3. Ukitambua, ukajituma Mungu akiweka kudra zake utafikia malengo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic