HUU NDIYO UJANJA WA MKONGOMANI YANGA KUWATUMIA MAWENZI MARKET LEO
Wakati kikosi cha Yanga kikishuka dimbani leo kuvaani na Mawenzi Marekt, mchezo ambao utakuwa wa kumuaga aliyekuwa beki wa kikosi, Nadir Haroub ' Cannavaro, Kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera ameweka bayana atakachakifuatilia kwenye mtanange huo.
Zahera ambaye anakinoa kikosi hicho Morogoro kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, amesema atawatumia Mawenzi kuangalia uwezo wa wachezaji wake kucheza kitimu.
Aidha, mbali na kucheza kitimu, Zahera amesema ataangalia pia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ili kuhakikisha mipira kwa wachezaji haipotei kirahisi, jambo ambalo anaamini litawasaidia kupambana na USM Alger.
Tayari Yanga imeshacheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kukabiliana na Mawenzi leo ambapo ilikuwa dhidi ya Tanzanite Academy na kuipa kipigo cha kufa mtu kwa kuitwanga mabao 5-1.
Ikumbukwe Yanga wameweka kambi ya wiki mbili mjini humo kujiandaa na mechi dhidi ya Waarabu hao huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa awali kwa mabao 4-0 huko Algiers.
0 COMMENTS:
Post a Comment