August 12, 2018


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Obrey Chirwa, ametoa ushauri kwa straia mpya wa Simba, Adam Salamba juu ya suala la upigaji wa penati.

Chirwa ambaye alicheza Yanga akiwa sehemu ya kikosi cha kwanza, ameamua kufunguka na kumtaka Salamba kuachana na upigaji penati kutokana na lawama za mashabiki wa soka la Tanzania.

Mzambia huyo amesema katika soka la hapa nchini mashabiki wa Yanga na Simba kufurahishwa na mchezaji ambaye kazi yake ni kufunga pekee na si kukosea hata mara moja.

Kauli ya Chirwa ilikuja mara baada ya Salamba kukosa penati ambayo alipiga katika mchezo wa kirafiki Jumatano iliyopita dhidi ya Asante Kotoko ndani ya dimba la taifa.

Aidha, Chirwa ameeleza hayo baada ya kupokea lawama kali zilizotoka kwa mashabiki wa Yanga juu ya kukosa penati kadhaa ambazo alibahatika kupiga wakati akiwa anaicheza timu hiyo.

Simba ilishindwa kutamba dhidi ya wakongwe hao wa ligi ya Ghana baada ya mechi kumalizika kwa sare ya bao 1-1 huku Salamba akikosa penati ambayo pengine ingeweza kuwapa penati Simba.

2 COMMENTS:

  1. Salamba hakwenda kupiga penalt kwa ajili ya kufunga bali alikuwa anajifundisha kupiga penalt. Penalt hazina ufundi sawa lakini pale Simba kuna wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kujiamini katika upigaji wa penalt. Mkude, Asante kwasi hata Kagere.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo ndo lawama zenywe alizosema chirwa mashabiki wa simba na yanga vichwa maji kabisa kuna lipi jipya kwny mpira

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic