Inafahamika vizuri kwamba televisheni zote za kianologia zilizimwa tangu Januari 1, 2013 nchini Tanzania. Na kwa miaka iliyofata, urushaji wa matangazo na vipindi vya ndani ukabadilika kuwa wa mifumo ya kidigitali hivyo kufanya ongezeko kubwa katika maudhui na vipindi. Star Media (Tanznaia) Limited.
Moja ya kampuni kubwa za kidigitali zenye vibali (MUX), inafuata maono na mpango wa kuhakikisha kila familia ya kitanzania inapata huduma ya luninga za kidigitali ambayo wanaweza kumudu kutazama. Star Media (Tanznaia) Limited ndiyo kampuni iliyotengeneza na kuendesha huduma kubwa zaidi ya matangazo ya kidigitali, huku ikirusha matangazo ya zaidi ya chaneli 20 za ndani.
Jitihada zote hizi zilifanya uhamiaji kwenye mifumo ya kidigitali kuwa rahisi, na vipindi vingi vya ndani vimeweza kuonyeshwa.
Hata hivyo, kutokana na mawasiliano hafifu na wateja pia kutofafanua vizuri juu ya bidhaa zetu, kumekuwa na baadhi ya mambo kuhusu luninga za kidigitali ambayo hajaeleweka vizuri. Jitihada zaidi inabidi zifanyike katika kuwaelewesha kuhusu matangaazo ya kidigitali.
Hasa upande wa chanelii za Bure (FTA), inahitaji kuelezewa kama ifuatavyo:
1: Watumiaji wote wanaweza kununua dikoda za FTA kwa bei ya kuuzia ambayo ni Tsh 89,000 kwenye maduka yetu na kwa mawakala wa Star Media (Tanzania) Limited, kama zinavyoonekana kwenye picha ya kwanza.
Baada ya kununua dikoda ya aina hiyo wateja wanaweza kutazama chaneli za Bure bila kulipia malipo ya kila mwezi. Watapata chaneli kuanzia 6 hadi 16 (Inategemea na sehemu ambapo kibali cha mwenye maudhui kinaruhusu). Hii pia ni hatua ambayo inayofatwa na Star Media (Tanzania) Limited kama kampuni yenye kibali (MUX).
2: Dikoda ya Kulipia inaweza kununuliwa kwenye maduka yetu na mawakala, kama inavyooneshwa kwenye kielelezo namba 2 hapo chini, dikoda hizi zina tozo ndogo ambayo watumiaji wanaweza kununua kwa gharama nafuu kisha wanalipia ada ya mwezi ili kutazama chaneli za bure za Nyumbani , na pia kutamzama chaneli nyingi zaidi za kimataifa na nyinginezo za nyumbani za kulipia. Gharama ya dikoda hii ni Shilingi 45000/=
3: Watumiaji pia wanao uwezo wa kuchagua dikoda nyingine tofauti kulingana na mahitaji yao. Pia kama mtumiaji aliyechagua dikoda ya kulipia akitaka kurudi/kubadilisha apate chaneli za bure sawasawa na mahitaji yake anaoweza kulipia tofauti ya gharama ambayo ni shilingi 44000 katika maduka yetu. Na baada ya hapo anaweza kutazama chaneli za bure.
Star Media (Tanzania) Limited taendelea kufanya kazi kisheria, bega kwa bega na TBC pia iataendeleza uhusiano mzuri na TCRA. Star Media (Tanzania) Limited itaendelea kuwapatia wateja wake huduma nzuri za luninga pamoja na kusaidia maendeleo ya tasnia ya luninga nchini Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment