KOCHA ALIYEIPA UBINGWA WA AFRIKA NIGERIA, ASAINI MIAKA MIWILI TAIFA STARS
Na George Mganga
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amemtangaza kocha Emmanuel Amunike kutoka Nigeria kuwa kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.
Kocha huyo amefikia mwafaka na TFF ya kusaini kandarasi ya miaka miwili kuinoa Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Serengeti.
Amunike aliwahi kutamba na kikosi cha Nigeria akicheza kama winga wa kushoto na pia alifanikiwa kuifundisha timu ya taifa hilo mwaka 1993 mpaka 2001.
Mchezaji huyo mstaafu alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1994 kilichowafunga Bulgaria mabao 3-0 katika hatua ya makundi na pia kupoteza dhidi ya Italy kwa mabao 2-1 kwenye 16 bora.
Aidha Amunike anakumbukwa kwa kuisaidia Nigeria kutwaa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1994 huko Tunisia na baada ya mashindano hayo aliweza kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika.
Huyu kweli ana hadhi ya kuifundisha timu ya taifa, KILA LA KHERI TAIFA STARS,KILA LA KHERI KOCHA AMUNIKE,
ReplyDeleteHuyu kweli ana hadhi ya kuifundisha timu ya taifa, KILA LA KHERI TAIFA STARS,KILA LA KHERI KOCHA AMUNIKE,
ReplyDeleteKwa kweli ukisikia sikio la kufa halisikii dawa basi ni Timu ya Taifa stars na TFF yake. Makocha wote hao duniani waliojaa wenye sifa stahiki leo wanakwenda kutuletea kocha ambae hakika hatatupeleka kokote kule. Ndio alikuwa mchezaji mahiri lakini masuala ya ukocha ni habari nyengine. Ndio amekuwa akifundisha timu za vijana kwa mafanikio lakini hapa tunazungumzia Taifa Stars sio Serengeti boys? Tukisema utasikia wahusika wanang'aka mwscheni kocha afanye kazi kwani kama ilivyokuwa kwa Ame Ninje ambao TFF na uongozi wao waliwahakikishia watanzania ni kocha wa kiwango wa Dunia nyengine kabisa. Hivyo Taifa Stars itakuwa timu ya kujifundishia ukocha mpaka lini?
ReplyDeleteUsiongee kwa hisia leteni hoja. Kwanza umesoma vizuri habari yenyewe na kuielewa au kwa kuwa umedhamiria kuponda tu? Makocha wangapi duniani wanatoka kufundisha timu za vijana na kwenda timu kubwa bila hata kuzifundisha timu za wakubwa ba wanafanya vizuri? Guardiola wakati anateuliwa kuwa kocha wa Barcelona alikuwa amefundisha timu gani kubwa duniani? Ziadane anatoka kuwa kocha wa vijana, anakaa kwenye benchi la ugundi kwa muda mfupi, anafukuzwa Mourihno yeye anachukua nafasi, kuna kocha gani kafanya aliyoyafanya Zidane?
DeleteTunazungumzia makocha wa timu ya taifa sio vilabu? Zidane,Guardiola,Mourihno kwanini wanagwaya kuchukua majukumu ya timu ya Taifa? Timu ya Taifa sio kitu cha michezo mchezo kwa kocha aneijielewa na kutaka kutunza heshima yenye rekodi stahiki kwenye kazi yake. Wapo waafrika makocha wenye uwezo na uzoefu mzuri tu kama hamu ilikuwa lazima tuwe na kicha muafrika. Waghana wana hazina kubwa tu ya makocha wenye uwezo na uzoefu mzuri hadi wa kombe la dunia.
ReplyDeleteMimi naona ndio maana hata hao wenyewe TFF walikuwa wanaogapa hata kumtangaza. Mchakato wa kutafuta kocha huyo ulifanywa kwa siri kwanini? Kwanini TFF wanashindwa kuwa wawazi na kuwashirikisha watanzania wengine hasa katika suala hili la kutafuta kocha.
ReplyDeleteMimi nikubali kwamba anon sifa zake huyu mocha ni za miaka mingi iliyopita. Unazungumzia 1993 mappa 2001. Hai mica 5 ya vivi karibuni alikuwa wapi na amefanya nini? TFF msipoturidhisha na uwezo wake kwa sasa ukoje kwakweli itakuwa kasoro kubwa.
ReplyDeleteMimi nikubali kwamba sifa zake huyu kocha ni za miaka mingi iliyopita . Unazungumzia 1993 mpaka 2001. Hivi hii miaka 5 ya hivi karibuni alikuwa wapi na anafanya nini? TFF msipoturidhisha na uwezo wake kwa sasa kwakweli itakuwa kasoro kubwa.
DeleteEbu tusiwe wakosoaji Sana tukaja kuumbuka tumpe ushirikiano huyo kocha afanye kazi yake
ReplyDeleteTatizo tumezoea ngozi nyeupe, weusi wenzetu hatuwathamini.
ReplyDelete