August 14, 2018


Baada ya mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu kuonekana akifanyishwa mazoezi peke yake tangu ajiunge na wenzake katika kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro, kocha mkuu wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amefungukia ishu hiyo.

Ajibu aliyejiunga na wenzake kambini tangu Jumatano ya wiki iliyopita, amekuwa akifanyishwa mazoezi ya peke yake na kocha msaidizi wa kikosi hicho, Noel Mwandila raia wa Zambia.

Yanga ambayo ilifika Morogoro takribani wiki mbili zilizopita, inajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Agosti 19, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar. Pia kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 22, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Championi, Zahera alisema kutokana na Ajibu kuchelewa kuingia kambini, ndiyo maana wameamua kumpa mazoezi yale ambayo wenzake walianza nayo.

“Ajibu alichelewa wiki moja wakati sisi tukiwa hapa, lazima awe sawa na wenzake ndiyo maana anafanya yale mazoezi ambayo wenzake walifanya wakati yeye hayupo.

“Siku zote unapojenga nyumba ni lazima uanze chini, ndiyo kama hivi tunavyomfanyia Ajibu, ili awe fiti kama wenzake ni lazima na yeye afanye yale mazoezi wenzake walianza kuyafanya,” alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic