August 31, 2018


Kiungo wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima imeelezwa kuwa ameuangukia uongozi wa klabu hiyo kwa kuandika barua ya kuomba msamaha na wakati wowote kuanzia sasa atajiunga na timu.

Niyonzima alishindwa kujiunga na kikosi cha Simba kwenye kambi ya nchini Uturuki katika maandalizi ya msimu huu kutokana na tofauti aliyokuwa nayo na uongozi wa klabu hiyo ambapo kwa sasa wameshamalizana.

Kiungo huyo ambaye alijiunga na Simba akitokea Yanga msimu wa 2017/18, alishindwa kupata nafasi kubwa ya kucheza msimu uliopita kutokana na kuwa majeruhi.

Habari za uhakika ni kuwa tayari Niyonzima amewasilisha barua ya kuomba msamaha na uongozi unalifanyia kazi suala hilo ambapo suala lake limepelekwa katika Kamati ya Maadili ya Simba.

5 COMMENTS:

  1. NIYONZIMA MSUMBUFU NA NI KIBURI SIMBA ACHANENI NAYE ATAWAHARIBU WACHEZAJI WENGINE KWENYE KIKOSI

    ReplyDelete
  2. Wasiwachane naye ila awe anatokea benchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asugue benchi mwanzo mwisho..!!

      Delete
  3. Very nice. The weak can never forgive. Forgiveness is the attribute of the strong

    ReplyDelete
  4. Huyo jamaa nizaidi ya komedi Kwani hayo yoteytumeyaona akiwa Mbute fc kwaiyo kuweni makini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic