August 10, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Simba kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Lindi kwa kambi ya siku kadhaa kuendeleza maandalizi ya msimu mpya unaitaraji kuanza Agosti 22.

Kikosi hicho kikiwa Lindi kitacheza mchezo mmoja wa kirafiki na Namungo FC katika Uwanja wa Majaliwa majira ya jioni.

Simba imeondoka Dar ikiwa ni siku moja imepita baada ya kukipiga na klabu kongwe kutoka Ghana, Asante Kotoko juzi Jumatano na kwenda sare ya bao 1-1.

Katika ufunguzi wa pazia la ligi, Simba itaanza kumenyana na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


5 COMMENTS:

  1. Naona simba inaenda kucheza na timu ya ligi kuu ya msumbiji hongereni sana simba kwa kuendelea kucheza na timu kubwa zenye majina waacheni yanga wanaocheza na timu za mchangani sijui Tanzanite

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mahusiano yet mazuri na timu za mkoa wa Lindi ni wajibu kuwapiga tafu ndio mahusiano Hongera Simba

      Delete
  2. Wakirudi ni lazima usikie fulani na fulani wameumia.. Fulani na fulani ni majeruhi hawatoweza kucheza kwa kipindi fulani..!!
    Kisa; viwanja vibovu vya mikoani...

    Najua wengi hawataelewa hoja yangu make pengine ipo mbali na upeo wa macho yao..
    Lakini TFF hii bado imeshindwa kusimamia ubora wa viwanja vyetu vya michezo.. Na hata wenye viwanja (ccm) nao hawajuhi nini cha kufanya na viwanja vyao..!!
    So shame..! Very bad..!!

    Simba nendeni tu mkacheze ila wapeni fursa hiyo vijana wa timu B na si akina Tripple C, emmosting, Bocco, MK14, AS10, manula, kichuya n.k!!
    Vijana nao ni wachezaji.. wapeni fursa wacheze..!!
    Be appropriately warned!!

    ReplyDelete
  3. Asante Simba kwa kujipima na vikosi vya heshima vilivochukuwa mataji makubwa badala ya vikosi vya wauza madafu ili muradi tu wapate ushindi wa kujidanganya wa kishindo. Simba imetulia kilakona huku wakiteleza uwamjani kama nyoka wakiwa na amani ya kila kitu



    ReplyDelete
  4. Simba wanaenda Lindi kwa heshima ya mwanachama mwenzao Kassim Majaliwa, ambaye amewaalika kwenye uzinduzi wa uwanja uliopewa jina la Majaliwa Stadium. Hiyo mechi ingefaa wacheze wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye mechi ya kimataifa dhidi ya Asante Kotoko. Tunahofia wachezaji wetu kuumia kwenye viwanja vyenye pitch mbovu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic