August 11, 2018


Kikosi cha Simba kimeshindwa kutamba mbele ya Namungo FC kwa kwenda suluhu ya 0-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Ruangwa, Lindi.

Katika mchezo huo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Majaliwa Simba walionekana kupata nafasi nyingi zaidi na kuonesha asilimia kubwa ya umiliki wa mpira japo nyavu zikashindikana kutikishwa.

Mech hiyo imepigwa Ruangwa ikiwa ni maalum kwa ajili ya kuuzindua Uwanja huo wa Majaliwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Baada ya mchezo huo, Simba wataendelea na mazoezi baada baada ya kesho kujiwinda na Mtibwa Sugar kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani.

Simba watakuwa wanakipiga na Mtibwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Agosti 18 baada ya kuutwaa ubingwa wa VPL 2017/18 huku Mtibwa wakichukua Kombe la Shirikisho.

4 COMMENTS:

  1. Kwa watu wa mpira tunasema mpira unamatokeo matatu ingekuwa yanga ndo kapata hayo matokeo puvu watu lingewatoka kama wao ndo wanauchungu na yanga

    ReplyDelete
  2. Tunazidi kuona mafanikio ya kambi ya uturuki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahaha si tunacheza September 30 VPL ? Tusubiri. Rangi halisi ya Simba itajionyesha siku hiyo.

      Delete
  3. Matokeo haya mazuri sana kwa kila upande umeweka heshima kwa mwenzake. Simba imepata heshima kuwa timu ya kwanza kucheza uwanja huo na wenyeji wao. Hongereni sana. Namungo imeweka heshima ya kucheza na kutoka sare na klabu bingwa ya Tanzania. Time hizi tayari wana mahusiano mazuri na inawajenga confidence wachezaji wetu wa Namungo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic