BAADA YA KUKIPIGA NA NAMUNGO, MAJALIWA ASHANGAZWA NA JAMBO HILI JUU YA SIMBA
Baada ya Simba kukipiga na Namuongo FC jana kwenye Uwanja wa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ameshangazwa na kikosi cha Simba kilichowasili mjini hapo.
Majaliwa amefunguka wakati akihutubia kabla ya mechi hiyo iliyokuwa maalum kwa ajili ya kuzindua Uwanja huo 'Majaliwa Stadium' akisema kuwa haijawahi kutokea kikosi kizima cha Simba kikasafiri na wachezaji wa kikosi cha kwanza kuelekea Wilayani.
Kiongozi huyo alisema hayo kutokana na uongozi wa klabu hiyo kupelekea kikosi cha kwanza ambacho pia wachezaji wake walicheza japo wengi wakiingia kipindi cha pili.
Simba iliwaingia Emmanuel Okwi, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya wakichukua nafasi za wale walioanza kipindi cha kwanza ili kunogesha zaidi uzinduzi wa Uwanja huo mpya.
Katika mchezo huo, mechi hiyo ilimalizika bila kupata mbabe kwa kwenda suluhu tasa ya 0-0.
NI KUONYESHA HESHIMA KUBWA SIMBA INAVYOHESHIMU KUANZIA VIONGOZI WAKE WAZIRI MKUU NA MKOA WOTE WA LINDI.
ReplyDelete