Yanga imesema lengo la kuandaa mechi pamoja na Bonanza Agosti 12 ni kwa ajili ya kumuaga nahodha wao kwa zaidi ya miaka 10, Nadir Harob ‘Cannavaro’.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amewaambia waandishi wa habari kwamba, watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mawenzi lakini kabla kutakuwa na tamasha hilo.
“Wasanii maarufu kama Afande Sele, Bill Nass na wengine watatumbuiza kwa kuwa tunataka kumuaga vizuri nahodha Cannavaro,” alisema.
Kwa sasa Cannavaro ni meneja wa kikosi cha Yanga ambacho amekitumikia kwa zaidi ya miaka 10 kwa mafanikio makubwa.
Yanga imeweka kambi yaje mjini Morogoro kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Duuh na mawenzi?
ReplyDeleteMawenzi timu ya wapi? Imo kwenye VPL?
DeleteMmhh kweli yajayo yanafurahisha....Mawenzi market tena!
ReplyDelete