September 8, 2018


Baada ya mchezaji Mohammed Issa Banka kuripotiwa amefungiwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa muda wa miaka miwili, mzazi wa mchezaji huyo ameibuka vikali na kuvitaka vyombo vya habari Zanzibar kuacha kumuandika vibaya mtoto wake.

Baba mzazi wa mtoto huyo ameibuka na kusema mpaka sasa hawana barua rasmi inayoleza kuwa Banka amefungiwa kwa muda huo, jambo ambalo kama wazazi hawalifurahii.

Mzazi huyo ametoa msisitizo kwa baadhi ya vyombo hivyo huko Zanzibar akivitaka viache mara moja kuandika taarifa za uzushi kuhusu mwanae bila kuwa na uhakika.

Aidha, Mzee huyo amewachana baadhi ya mashabiki wa Yanga mjini humo baada ya kuanza kumtupia lawama Banka kuwa amekula fedha za Yanga kutokana na kutoichezea timu hiyo mpaka sasa.

Mashabiki hao walieleza kuwa walimchangishia fedha Banka baada ya kujiunga Yanga lakini mpaka sasa hayupo kikosini kitu ambacho kimewafanya wacharuke na kuanza kumtupia lawama kuwa amekula fedha za bure.

Kitendo hicho kimezidi kumuumiza zaidi baba mzazi wa Banka na kuzidi kutema cheche akiwataka waache mara moja kumsingizia mwanaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic