SIMBA WASHANGAZWA NA WACHUKUA FOMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Na George Mganga
Ikiwa imetolewa wiki moja pekee kwa ajili ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Simba kuchukua fomu, uongozi wa klabu hiyo umesema spidi ya wachukua fomu imekuwa ndogo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema mpaka sasa wachukua fomu wamekuwa wakisitasita tofauti na ambavyo walikuwa wakitarajia hapo awali.
Manara ameeleza inapaswa wale wote walio na vigezo stahiki wajitokeze kunako makao makuu ya klabu mitaa ya Msimbazi, Kariakoo kwa ajili ya kuchukua fomu hizo ili kusubiria zoezi la uchaguzi.
Ofisa huyo amesisitiza kwa kuwataka wanachama hao wajitokeze haraka kuchukua fomu hizo kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu utakaofanyika Novemba 3 2018.
Wakati huo Simba leo inashuka dimbani, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya kuanzia mida ya saa 12 jioni.








0 COMMENTS:
Post a Comment