September 2, 2018


Unaweza usiamini lakini ndiyo imetokea. Yule straika hatari aliyekuwa akiichezea Yanga, Obrey Chirwa, ametuma maombi kwa mabosi wa klabu yake ya zamani akiomba arejee.

Imeelzwa Chirwa ametuma ujumbe huo kwa njia ya sauti kupitia mtandao akiuomba uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, umpe nafasi ya kurejea.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Chirwa amesema huko alipo Misri mpaka sasa hajapewa fedha zake za usajili na timu anayoichezea hivyo anaweza akavunja mkataba muda wowote.

Aidha, taarifa imeeleza huko anakochezea ni mbali na kwao Zambia hivyo kama akirejea hatakuwa na ugumu wa kusafiri kuelekea kwao kutokana na umbali kutokuwa mrefu.

Mchezaji huyo aliondoka Yanga na kutimkia Uarabuni baada ya kushindwa kufikiana mwafaka na mabosi wake wa zamani kuongeza mkataba mwingine.

8 COMMENTS:

  1. Ukome...
    Rudi ymbn kumenoga mwana mpotevu

    ReplyDelete
  2. Huyo hatakiwi kurudishwa. Aligoma kucheza mechi muhimu timu imeharibikiwa lakini yeye mshahara wake kalipwa. Je hasara aliyotutia kwa kukataa kwenda Algeria na kuondoka wakati tunajiandaa kucheza na Gor Mahia anailipa nani? Labda kama viongozi wa Yanga wanatak ausumbufu wake lakini kwa maana ya mchezaji CHIRWA hapana. Ameweka mbele pesa kuliko utu. Hata huko kwakuwa hajalipwa je angelipwa amgeikumbuka Yanga? Aende zake huko

    ReplyDelete
    Replies
    1. kipaji cha Chirwa na uwezo wake uwanjani ni muhimu kwa yanga........mkosaji anasahihishwa makosa yake au yeye mwenyewe anajifunza kutokana na makosa then maisha yanaendelea.

      Delete
  3. Habari zingine ni majungu matupu! Ushahidi anao unesha kwamba anataka areje Yanga uko wapi? Hivi unadhani Chirwa anakosa timu ya kuchezea mpaka arudi jangwani tu? Acheni uandishi ushwara wa kupotezea wasomaji muda. Taja chanzo cha habari yako sio kuandika kama vile unaandika udaku.

    ReplyDelete
  4. UONGOOOO....eti katuma ujumbe wa sauti kupitia matandao!

    ReplyDelete
  5. Waongoooo nyieee mmemxhindwa ss mnamtaka tena Kweli nyiee mbute

    ReplyDelete
  6. Namtamani sana O'Brien Chirwa. Kama angekuja akatengeneza pacha na Makambo, mambo yangenoga sana. Tatizo lake ana mashauzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic