September 8, 2018


Kiungo mpya wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amefunguka kuwa atatumia nguvu na jitihada zake zote kuhakikisha anakilinda kiwango chake ili aendelee kuwa bora zaidi kwenye ligi.

Fei Toto amekuwa akionyesha kiwango kizuri tangu alivyotua klabuni hapo kutokana na soka safi analolionyesha kiasi cha kuibua matumaini mapya kwa Yanga msimu huu.

Fei Toto amesema kuwa, anahitaji kujituma zaidi mazoezini ili kuweza kulinda kiwango chake ili aweze kufanya vizuri zaidi katika timu yake.

“Ili kiwango changu kiendelee kuwa bora zaidi, ni muhimu kujitunza na kujielewa katika kujituma mazoezini na kusikiliza anachofundisha mwalimu.

“Kuhusu kuendelea kuwepo katika kikosi cha kwanza hilo ni jukumu la mwalimu ambaye ndiye mwenye maamuzi ya kuchagua ampange nani katika kikosi cha kwanza.

“Nikizungumzia kuhusu ligi ni ngumu na inaushindani mkubwa hivyo tunahitaji kujituma zaidi ili tufanye vizuri,” alisema Fei Toto.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic