September 8, 2018


Na George Mganga

Wakati wadau wengi wa soka hapa nchini na Uganda wakisubiria kwa hamu pambano baina ya mataifa hayo mawili kati ya Uganda The Cranes dhidi ya Taifa Stars, inaelezwa vuguvugu la kisiasa linaweza kuwatoa waganda mchezoni.

Taarifa za ndani kutoka Kampala zinasema kutokana na kutokuwapo na hali shwari ya kisiasa nchini humo inawezekana kwa namna moja ama nyingine inaweza ikaathiri hamasa na shamrashamra za mechi hiyo kwa waganda.

The Cranes inaenda kuchuana na Stars ikiwa imegubikwa na matukio kadhaa ya kisiasa ikiwemo sakata la Mwanasiasa na Mwanamuziki Robert Kyagulanyi 'Bob Wine' ambaye yupo nchini Marekani kwa matibabu.

Aidha, ukiachana na Bob Wine baadhi ya matukio mengine yameripotiwa kuchagiza kwa kupoteza mvuto wa mechi hiyo ambayo inafanyika leo kwenye Uwanja wa Mandela.

Licha ya uwepo wa matukio hayo, tayari timu zote mbili zilishaamilisha maandalizi kwa ajili ya kukipiga ambapo katika kund L Uganda ipo kileleni ikiwa na alama tatu huku Stars na Lesotho zikiwa na alama 1 kwa kila mmoja.


5 COMMENTS:

  1. Hapa ndio Mara nyingi na kuwa sina imani na wachambuzi wa mpira Tanzania sijui issue huwa wanaziona vipi tukifungwa mtasema tumekufa kiume

    ReplyDelete
  2. Uchambuzi au ujinga tu.Badala ya kuleta uchambuzi wa kitaalamu wanatuletea utabiri wa marhum Sheikh Yahya Husein.Tunashangaa nini wakati huo ndio mwisho wa uwezo wao wa kufikiri.

    ReplyDelete
  3. Mpira wetu haupandi kutokana na aina hii ya uchambuzi ambao unaonyesha una nia ya kutuaminisha kupata ushindi kwa ulaini mwisho wa siku tunapoteza match, tujitafakari.

    ReplyDelete
  4. Duuuuu.
    Hii blog ina brand kubwa ila waandishi wanaiangusha sasa nini hiki kakiandika huyu George Mganga yani ni sawa na Ali kiba au Diamond awe na mgogoro na serikali zen Taifa Stars ifungwe kwa kuwa Kiba ana mhogoro au kapigwa na jeahi la polisi.Hapo kuna uhusiano gani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic