UONGOZI YANGA WAVICHANA VYOMBO VYA HABARI, WATOA ONYO
Na George Mganga
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu, Omar Kaya, umevitaka baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za uzushi na uongo unaoihusu timu yao.
Kaya amesema imefikia hatua baadhi ya vyombo hivyo viweke wazi ueledi badala ya kuzidi kuandika habari ambazo zimekuwa hazina mashiko zenye uwezekano wa kuiharibu taswira ya klabu.
Kaimu huyo ameeleza kuwa si jambo la busara kufanya hivyo kwa maana inaweza ikawagombanisha na baadhi ya taasisi zingine kitu ambacho kitaleta sifa mbaya kwa klabu.
Kaya ametolea mfano wa taarifa ambayo ilichapishwa na baadhi ya vyombo vya habari ikieleza kuwa kuna wachezaji wake kadhaa wamepelekwa kwenye Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya kuhojiwa akisema haikuwa na ukweli wowote.
Kiongozi huyo amewataka mashabiki, wapenzi na wanachama na wadau wote wa mpira kupuuzia taarifa hizo pamoja na zote ambazo zimekuwa zikiandikwa kwa lengo la kuichafua Yanga wazipuuzie.








0 COMMENTS:
Post a Comment