KOCHA AZAM ATAKA POINTI 9 KWA TIMU HIZI
Kocha Mkuu wa Azam FC, Mjolanzi, Hans van der Pluijm, ametamba kuondoka na pointi 9 kanda ya ziwa ambapo timu yake itakuwa na mechi tatu.
Pluijm ameeleza kuweka mikkakati hiyo ili kujiwekea nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa msimu huu ambao unatetea na Simba walioutwaa 2017/18.
Kikosi cha Azam kitasafiri kuelekea Shinyanga tayari kukipiga na Mwadui FC Septemba 14 kisha Biashara United ya Mara Septemba 19.
Baada ya hapo Azam watakuwa wana kibarua kingine dhidi ya Alliance ya Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Septemba 24.
Kocha huyo amesema anaufahamu vizuri upinzani na ugumu wa mechi za kanda ya ziwa hivyo atahakikisha anakiweka kikosi vizuri ili kukipa ushindi kujiwekea mazingira mazuri ya kuuchukua ubingwa wa ligi.








0 COMMENTS:
Post a Comment