September 9, 2018


Wakati ligi ikiwa imesimama kwa muda ambapo ilikuwa ikipisha mechi za kitaifa, uongozi wa Coastal Union umesema unaendelea kujifua vilivyo kujianaa na mechi zijazo.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda, amesema wao gari lao halijazima na kinachoendelea hivi ni kurekebisha mapungufu yaliyojiktokeza mechi zilizopita.

Mgunda ameeleza kuwa sasa anapambana kutengeneza makali haswa katika safu ya beki na ushambuliaji ili kuiweka timu sawa kwa ajili ya kupata matokeo.

Vilevile, Mgunda amewapa tahadhari wapinzani wote kwenye ligi akiwataka wajiandae kuupata moto kwani wapo kwa ajili ya ushindani na si kushiriki ligi pekee.

Aidha, Mgunda amemtaja straika wake Ali Kiba kuwa sehemu ya mechi ijayo baada ya kuzikosa mechi zote za mwanzo kutokana na kuwa na majukumu mengine kimuziki.

Kiba tayari ameshaanza mazoezi na Coastal Union kujiandaa na mechi zijazo ambapo kuelekea mchezo ujao atakuwa dimbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic