MANARA AAHIDI KUWASHANGAA MASHABIKI SIMBA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki wake na watanzania kwa ujumla kuipa sapoti Taifa Stars ambayo inacheza kesho dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON 2019.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema watanzania wote wanapaswa kuwa kitu kimoja kwa kuonesha utaifa na uzalendo kwa Stars ambayo itakuwa inaiwakilisha nchi.
Aidha, Manara amesema atawashangaa mashabiki baadhi wa Simba ambao wataipa sapoti Uganda kutokana na kuondolewa kwa wachezaji wake 6 kwenye kikosi cha Stars kutokana na kuchelewa kufika kambini akieleza kuwa ni sababu ambayo haina maana.
Manara pia amefunguka kwa kusema sababu ya uwepo wa wachezaji wao Juuko Murushid na Emmanuel Okwi kwenye kikosi cha Uganda, isiwe sababu ya kuikacha Stars na badala yake akiwataka waweke utaifa mbele.
Mbali na kuipa hamasa Stars, Manara amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho ambapo timu yao itakuwa inacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya majira ya saa 12 jioni.
Sanjari na kujitokeza Uwanjani, mashabiki hao pia ambao watawahi watapata fursa ya kuutazama mchezo wa Uganda dhidi ya Stars ambao utarushwa mbashara kupitia kituo cha ZBC 2.








manara huwa anajipa majukumu makubwa yasiyomhusu, swala la kushabikia ni la washabiki wenyewe wala sio la manara.hakuna shabiki mzalendo wa simba atakayeshabikia uganda labda tu kama yanga ingekuwa inacheza
ReplyDeleteWatu wengine mabumbula kweli kweli. Yaani kuna baadhi ya watanzania wao kazi yao kupinga tu yaani neno upinzani limeingia katika vichwa vya baadhi ya watanzania nakuwa maradhi kuviozesha vichwa vyao kutokuwa na uono wowote isipokuwa kupinga kila kitu. Katika jamii ya kitanzania kuna magonjwa mawili hatari makubwa yanayowatafuna Watanzania Ukimwi na upinzani wa mambo hata kama ya msingi. Manara ni msemaji wa Simba na ni miongoni mwa watu wa Simba wenye ushawishi mkubwa kwa wanachama na wapenzi wa klabu hiyo. Sasa leo anawahimiza wanasimba kuisapoti timu ya Taifa Stars mtu anampinga? Sasa kama si chuki binafsi kitu gani? Sio siri wanachama na wapenzi wa Simba wanadonge la roho kwa kuzalilishwa wachezaji wao kufukuzwa timu ya Taifa kimizingwe kwa kisingizio cha nidhamu wakati wachezaji hao ni miongoni mwa wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu na kujitoa kwa nguvu zao zote kwa timu ya Taifa. Vipi utasema John Boko na Shomari kapombe hawana nidhamu kwa timu ya Taifa ?
ReplyDeleteNi kwel wa🇹🇿🇹🇿 lazma tujitathamin wenyew coz hai make sense kuacha kuwashangilia Watanzania na kwenda kuwashabikia Waganda kwanza watatuo maana
ReplyDeleteOchuu wa Mtwara
ReplyDeleteWatanzania 🇹🇿🇹🇿 tusiwe HV kwa kip Leo tuache kushabikia Taifa letu na kwenda Uganda kwanz waganda wenyew watatuona
Sie hatujitambui so tubadilike
Fact mzee baba Ochuujunior@gmail.com wa Mtwara
Delete