September 9, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa anaamini mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere ana ubora zaidi kuliko mshambuliaji wa Yanga, Haritier Makambo.

Kagere ndiye kinara wa mabao ligi kuu akiwa katupia matatu katika michezo miwili ambayo timu yake imecheza, Makam­bo yeye ana bao moja alilo­tupia katika mchezo mmoja ambao timu yake imecheza kwenye ligi kuu.

Aussems ambaye analipwa mshahara wa Sh milioni 22.7 kwa mwezi Simba, ameliam­bia Championi Jumamosi kuwa, kutokana na Kagere kutimiza vizuri majukumu yake ya kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha tofauti na washambuliaji wengine, anaamini ndiye bora na hakuna wa kumfanani­sha naye.

“Sioni haja ya kuongelea mchezaji mmojammoja lakini kwangu naona Kagere ni mchezaji mzuri zaidi kwa kuwa amekuwa akitimiza maju­kumu yake ya kufunga na kuonye­sha ubora wake vizuri tofauti na washambuliaji wengine.

“Naona anafanya kazi kubwa kutokana na jukumu ambalo analo, timu yote inamtegemea kuweza kuleta ushindi na ndiyo maana nasema ni bora zaidi kwa kuwa yeye kazi yake ni ku­hakikisha anafunga mabao.

“Kuhusu Makambo, namjua kwa sababu ni mchezaji mwenye miguu miwili hawezi kumfikia Kagere,” alisema Aussems.

6 COMMENTS:

  1. Acheni unafiki wekeni matokeo ya Simba na AFC Leopards! Au ndio mnasubiri kesho kuandika habari yenye kichwa "Kikosi cha mauaji cha Yanga"

    ReplyDelete
  2. FAKE NEWS.habari za uongo

    ReplyDelete
  3. KOCHA HAWEZI KUSEMA MANENO HAYO UONGO MNATENGENEZA HABARI WENYEWE

    ReplyDelete
  4. Habari kama hii ndio kiwango cha saleh Jembe hivi sasa.Mmeenda chini mpaka inatia aibu sans.Mlishaona sisi wasomaji wenu ni watu wa kupokea habari za takataka!Sivyo eh?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic