MBELGIJI SIMBA AMTAJA STRAIKA YANGA ALIYEZIDIWA NA KILA KITU NA KAGERE
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa anaamini mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere ana ubora zaidi kuliko mshambuliaji wa Yanga, Haritier Makambo.
Kagere ndiye kinara wa mabao ligi kuu akiwa katupia matatu katika michezo miwili ambayo timu yake imecheza, Makambo yeye ana bao moja alilotupia katika mchezo mmoja ambao timu yake imecheza kwenye ligi kuu.
Aussems ambaye analipwa mshahara wa Sh milioni 22.7 kwa mwezi Simba, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kutokana na Kagere kutimiza vizuri majukumu yake ya kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha tofauti na washambuliaji wengine, anaamini ndiye bora na hakuna wa kumfananisha naye.
“Sioni haja ya kuongelea mchezaji mmojammoja lakini kwangu naona Kagere ni mchezaji mzuri zaidi kwa kuwa amekuwa akitimiza majukumu yake ya kufunga na kuonyesha ubora wake vizuri tofauti na washambuliaji wengine.
“Naona anafanya kazi kubwa kutokana na jukumu ambalo analo, timu yote inamtegemea kuweza kuleta ushindi na ndiyo maana nasema ni bora zaidi kwa kuwa yeye kazi yake ni kuhakikisha anafunga mabao.
“Kuhusu Makambo, namjua kwa sababu ni mchezaji mwenye miguu miwili hawezi kumfikia Kagere,” alisema Aussems.








Acheni unafiki wekeni matokeo ya Simba na AFC Leopards! Au ndio mnasubiri kesho kuandika habari yenye kichwa "Kikosi cha mauaji cha Yanga"
ReplyDeleteHii leo
DeletePengine ile mechi hawakuangalia.Biasness!!!...
DeleteFAKE NEWS.habari za uongo
ReplyDeleteKOCHA HAWEZI KUSEMA MANENO HAYO UONGO MNATENGENEZA HABARI WENYEWE
ReplyDeleteHabari kama hii ndio kiwango cha saleh Jembe hivi sasa.Mmeenda chini mpaka inatia aibu sans.Mlishaona sisi wasomaji wenu ni watu wa kupokea habari za takataka!Sivyo eh?
ReplyDelete