September 13, 2018


Staa wa muda mrefu katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ hivi karibuni yamemkuta mazito akiwa baa baada ya watu wasiojulikana kumuwekea vitu vilivyodaiwa ni madawa ya kulevya kisha kumuibia kila kitu.

Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina kilitutonya kuwa, siku ya tukio Johari alifika katika baa hiyo iliyopo maeneo ya Sinza jijini Dar na kuanza kupata kinywaji akionekana kama aliyekuwa akimsubiria mtu.

“Akiwa anaendelea kupata kinywaji, kuna watu walikuja wakakaa pembeni yake, mimi sikuwajua ni akina nani. Kuna wakati Johari alienda chooni, aliporudi sikujua kilichoendelea ila nilishangaa kumuona kama amesinzia hivi na wale watu wa pembeni yake sijawaona.

“Baadaye mwenyewe alipozinduka alijikuta hana pochi. Alichanganyikiwa na pombe yote ilimuishia, sisi tulihisi aliwekewa madawa ya kulevya na ndipo akafanyiwa mchezo huo,” alitiririka sosi huyo.

Katika kupata undani wa ishu hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Johari ambapo alipopatikana alisema kuwa, ni kweli alikumbwa na balaa hilo lakini anamshukuru Mungu aliachwa salama licha ya kuibiwa pochi iliyokuwa na vitu mbalimbali.

“Walionifanyia ule mchezo hata siwajui lakini namshukuru Mungu niko vizuri, wamenichukulia pochi yangu iliyokuwa na simu, pesa na vitu vingine, nilienda kutoa taarifa polisi na taratibu za kisheria zinaendelea,” alisema Johari.

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi la watu wanaolewesha watu kisha kuwaibia hivyo gazeti hili linawatahadharisha wasomaji wake kuwa makini katika kila eneo wanalokuwa ili kuepukana na majanga kama yaliyomkuta staa huyo.

3 COMMENTS:

  1. Hasemi ukweli, wasanii wanapenda ofa na vitu vya bure...
    Hakuna dawa wala nn, alilewa tu watu wakabeba mazaga... ana bahati ajaenda kuliwa

    ReplyDelete
  2. Kama kweli mambo hayo yapo kwanini sehemu zote za mkusanyiko kama baa,restaurant,supermarket,banks nakadhalika siziekewe kamera CCTV? ni kitu rahisi kabisa.

    ReplyDelete
  3. Mambo hayo ndugu zangu yapo na ni jambo la kuchukua tahadhari nalo kwasababu wala sio lazima uwe unapenda ofa havanna. Muhimu ni kukilinda kinywaji chako. Dada yangu na shemeji yangu hawanywi kilevi lakini waliwekewa kwenye juice kwenye sherehe ya harusi kwenye meza waliyokaa. Waliibiwa simu, dhahabu zao, mikufi mpaka pete. Ilividi walazwe hospitali siku mbili na kuwekewa dripu. Jambo baya sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic