September 7, 2018


Baada ya kocha wake Mwinyi Zahera kumsifia kuwa ana dhahabu miguuni mwake ingawa hajui kuzitumia, mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amefunguka kuwa kwa sasa yuko vizuri na yupo tayari kupambana.

Ajibu amefanya vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni hadi kufikia hatua ya kusifiwa na kocha wake huyo raia wa DR Congo.

Msimu uliopita, Ajibu alifanikiwa kufunga mabao saba huku mechi za mwishoni mwa ligi hiyo nyingi akikosa kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Championi Ijumaa, mshambuliaji huyo alisema kuwa anaendelea kujifua kuhakikisha anakuwa fiti kuweza kuipambania Yanga.

“Nashukuru Mungu binafsi naendelea vizuri na sasa nafanya mazoezi kwa ajili ya kupambana zaidi kwa sababu ndiyo kwanza msimu umeanza, hivyo ni vyema kuanza vizuri tangu mwanzo,” alisema Ajibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic