MSHAMBULIAJI YANGA: SIMBA MJIANDAE KISAIKOLOJIA
Amissi Tambwe amewataka mashabiki wa Simba wajiandae kisaikolojia ili yasije kutokea kama yale yaliyotokea Oktoba 1, 2016 katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza msimu wa 2016/17.
Katika mchezo huo ambao Simba waliingia uwanjani wakijiamini kuibuka na ushindi, iliwachukua dakika ya nane tu kupata bao la kuongoza kupitia kwa Shiza Kichuya jambo ambalo lilizua nderemo na vifijo.
Hata hivyo katika dakika 26, Tambwe alisawazishia bao hilo ambalo kabla ya kufunga aliushika mpira kisha akakwamisha wavuni jambo ambalo lilizua balaa uwanjani hapo na kujikuta mashabiki wa Simba waking’oa viti na kuanza kuvirusha ndani ya uwanja.
Tambwe alisema; “Kwa jinsi hali ilivyo sasa mashabiki wa Simba wanaamini kuwa watatufunga, lakini mpira hauko hivyo niwaombe tu wajiandae kisaikolojia na wakae wakijua kuwa lolote linaweza kutokea.”
“Msimu wa 2016/17 nilipoifungia timu yangu bao la kusawazisha ambapo kabla ya kufunga bao hilo wakati napokea pasi ya Mbuyu Twite bahati mbaya mpira ulinigonga mkononi baada ya kusukumwa na Novatus Lufunga lakini mwamuzi hakuniona na mimi nikaukwamisha mpira wavuni, hakika jambo hilo liliwaumiza sana Simba, lakini hivyo ndivyo mpira ulivyo, wajiandae kukubaliana na kila kitu kitakachotokea uwanjani,” alisema Tambwe.
Anachonga na yuko benchi. Angecheza ingekuaje?Ulicheza netiboli bado unajisifia?Kubwa jinga.
ReplyDeleteTunashukuru kwa ukiri wako kwamba nikweli uliushika.ahsante sana.
ReplyDeleteTunashukuru kwa ukiri wako kwamba nikweli uliushika.ahsante sana.
ReplyDeleteTimu yangu ya Yanga leo mmenipa presha .Mpaka niliomba mpira uishe.Kwa kweli inabidi tutafute plan B.
ReplyDeleteYanga hakuna timu
ReplyDeleteYanga hakuna timu
ReplyDeletePresha Presha nilikwenda msalani zaidi ya mara tano.Bila ya kuficha ukweli leo Simba alitupelekesha ile mbaya. Nilitamani kuzima TV.
ReplyDelete