September 30, 2018


Shabiki kindakindaki wa Simba, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro na msanii wa muziki wa HipHop, ametamba kwamba Meddie Kagere atamaliza mchezo wa leo.

Kagere mwenye mabao manne kwenye ligi baada ya kucheza michezo mitano amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa Msimbazi hali iliyopelekea wengi kuiga staili yake ya kuziba jicho leo atakuwa uwanjani akivaana na watani zake Yanga ambao wao wanamtegemea Herieter Makambo.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Jay alisema; “Uwepo wa fundi Kagere pale ndani ya Simba unanifanya nisiwe na mashaka na chama langu.”

“Ila mahitaji yetu makubwa ni kuona timu yetu inafanya kweli hasa katika ligi kuu na wakiendelea kupata matokeo mazuri maana yake tunajiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa msimu huu tunawaamini wachezaji wetu wasituangushe,” alisema Jay.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic