Hassan Dalali ambaye ni miongoni mwa wazee wanaoheshimika Simba, anasema; “Yanga tumewafunga kabla ya mechi kuchezwa, wana hofu, hivyo tunahitaji kuwa kitu kimoja ili tuweze kuchukua pointi tatu muhimu.”
Lakini Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali anasema ; “Kwa sasa sina hali ya kuufuatilia wala kuzungumzia mchezo wa Simba na Yanga, sijiwezi naumwa sana watu wote wanajua.”
Ila aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King Mputa’ amesema kuwa anaiona nafasi kubwa kwa mshambuliaji Meddie Kagere kuifunga Yanga leo Jumapili kuliko Heritier Makambo kuifunga Simba.
Kibadeni anasema; “Itategemea na jinsi watakavyoamka lakini kwa upande wangu nampa nafasi kubwa Kagere kuifunga Yanga bao hata moja ijapokuwa hawezi kufikia rekodi yangu ya ‘hat trick’.”
“Simba na Yanga mara nyingi zikikutana atakayeshinda ndio anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa wa msimu.”
Kocha wa Simba, Patrick Aussems anasema Msaidizi wake, Masoud Djuma ameimaliza Yanga nje ya uwanja baada ya kumkabidhi ripoti ya aina ya uchezaji wao.
“Naijua vizuri Yanga kupitia msaidizi wangu Djuma ambaye amekuwa akiifuatilia katika mechi tatu zilizopita hivyo amenieleza kila kitu juu ya wapinzani wetu na ninafanyia kazi.”
Lakini Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema; “Hatuna presha kabisa na mchezo huu, nawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kuja kuangalia mechi, nimewaambia wachezaji wangu wajitume ili tupate ushindi.”
CHANZO: SPOTI XTRA
0 COMMENTS:
Post a Comment