September 13, 2018


Siku za mshambuliaji wa Yanga Mkongomani, Heritier Makambo za kuendelea kubaki kukipiga Jangwani huenda zikawa zinahesabika baada ya baadhi za klabu za nje ya nchi kupiga hodi kuwania saini yake.

Makambo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga msimu huu wa Ligi Kuu Bara baada ya kocha mkuu wa timu hiyo raia wa DR Congo, Mwinyi Zahera kumpendekeza kutokana na kuvutiwa naye kwenye majaribio.

Mshambuliaji huyo hadi hivi sasa tayari amefunga mabao nane tangu ajiunge na Yanga kati ya hao mawili ya mashindano na mengine sita katika michezo ya kirafiki.

Inaelezwa tayari mawakala watano kutoka kwenye nchi tatu za Uarabuni na mbili za Ulaya ikiwemo Sweden na Norway wameshaonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.
Mtoa taarifa huyo alisema, mawakala hao wamemfuata mchezaji huyo na kuwapa maelekezo ya kuzungumza na viongozi kabla ya kumfuata yeye kutokana na kubanwa na mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga.

“Uwezekano wa Makambo wa kudumu kwa kipindi kirefu kuendelea kuichezea Yanga ni mdogo sana ni baada ya baadhi za klabu kutoka nje ya nchi zikiwemo za Uarabuni na Ulaya kuonyesha nia ya kumsajili.
“Huo mkataba wenyewe wa miaka miwili aliosaini Yanga sijui kama ataumaliza kutokana na yeye mwenyewe ndoto alizoziweka za kupiga hesabu ya kucheza soka Ulaya.”

Alipotafutwa Makambo kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Mimi ni mchezaji mwenye ndoto nyingi ikiwemo ya kucheza soka la kulipwa ambayo ni lazima niitimize nikiwa Yanga.

“Zipo baadhi za klabu zinaonyesha nia ya kunihitaji kwa kunipa ofa kutoka nje ya nchi ambazo nimewaambia nina mkataba na Yanga, hivyo vema zikafanya mazungumzo nao kabla ya kuja kwangu,” alisema Makambo aliyeibuka kuwa kipenzi cha Yanga.

CHANZO: CHAMPIONI

6 COMMENTS:

  1. Kwa uboragan alionao huyo mama wakambo. Au mnataka kumpaisha2 kiaina

    ReplyDelete
  2. Hamna lolote kwenye hii habari yule Chirwa Yanga walichonga anakwenda Ismailia hivi sasa yupo kitimu cha daraja pili anacheza bure hata kulipwa halipwi. Yanga walishabikia zaidi Chirwa kuondoka hapa kuliko kusajiliwa na Simba. Na kama SIMBA watajiridhisha kuwa Makambo ni mchezaji a kweli basi hana cha uarabuni au Ulaya atatua Msimbazi Yanga watake wasitske.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli wewe ni Bwege mtozeni, povu la nini huu ni mpira kaka waache watu na mabo yao!

      Delete
  3. Ukisikia ufa... Ndio mnao nyinyi mliocomment kila kitu simba wacheni ushabiki maandazi nynyi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mamndazi wewe mwenyewe HIV kwa akili yako unaona mama wakambo nimchezaj mzr huyo wakwenda kucheza uarabun kwa kiwango gan alichonacho

      Delete
  4. Haijacheza Mechi nyingi hazifiki tank za kuonyesha ubora....tatizo LA Saleh Jembe ni kunogesha habari za Jangwani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic