January 15, 2021

 


FISTON Abdulazack raia wa Burundi amemalizana na mabosi wa Klabu ya Yanga ili kuongeza makali Kwenye safu ya ushambuliaji. 

Abdulazack ambaye ni mshambuliaji yeye ni mshambuliaji ambaye anacheza pia timu ya Taifa ya Burundi.

Nyota huyo aliletwa duniani Septemba 5, 1993 ana umri wa miaka 27 anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo ikielezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili.

Walianza na Saido Ntibanzokiza kisha ikafuata Dickson Job na sasa ni zamu ya Abdulrazak.

Nyota huyo pia amewahi kucheza ndani ya Klabu ya ENPPI ya Misri ambapo jezi yake namba anayoipenda ni 12.

Kwenye timu ya Taifa ya Burundi amecheza jumla ya mechi 49 tangu msimu wa 2009 na ametupia mabao 19.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa lengo kubwa la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambulia ni kufunga mabao zaid.


18 COMMENTS:

  1. Warundi wameanza kuletana hawa jamaa bwana hawatupani kutafutiana ulaji. Kuanzia Ndayiragije akiwa Mbao,kule Namungo na sasa Yanga tena.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa tu we unaogopa nini mpira ni kazi acha ubaguzi wa rangi

      Delete
  2. Kocha Mrundi ataachaje kujaza warundi wenzake

    ReplyDelete
  3. Soka la Tanzania limekuwa ni gulio la wachezaji toka nchi jirani hata kama uwezo wao ni mdogo kuliko wazawa lakini wanapewa umuhimu mkubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulia wewe....mpira ni uwezo na Ujuzi wa mchezaji kama uwezo mdogo tafuta wenye uwezo

      Delete
  4. Kwanini usijadili chikwenda ,wenye uwezo wapi wapi?

    ReplyDelete
  5. ukishindwa kushindana naye ungana nae, hongera sana warundi kwa kujituma na ndo maana mnatawala soka la bongo kuanzia kocha wa timu ya Taifa (stars) na hata vilabu .

    ReplyDelete
  6. Wanatuzidi hata Elimu sisi tunajua tu Eng/Swahili ,Kagere anatawala Ligi anavyotaka si Mnyarwanda au akija Yanga ndo katoka jirani

    ReplyDelete
  7. Hongera ila Yanga hawajatatua tatizo kubwa kwenye kiungo hakuna ubunifu na utengenezaji wa nafasi za kufunga. Mabeki pia wa pembeni ni wale wanaocheza kizamani kukaba tu na hawapandishi team au kupiga krosi kwa ajili wa washambuliaji

    ReplyDelete
    Replies
    1. tutatatua tukishabeba ubingwa more sexy footie is coming primamry objective sasa ni kukuchapa na kuchukua ubingwa. Period.

      Delete
  8. Watu wanaangalia Uwezo, Sasa kwann uchukue mtu kwa kisingizio cha uTz lkn Hana uwezo, ndio wachezaji wetu wapambane, wasibweteke, mchezaji kama Ajibu angekaza sasaiv angekuwa mbali lkn ndio hivyo tena

    ReplyDelete
  9. Mimi Simba nawapongeza utopolo(utani tu msimaindi) kwa kusajili Ila asije akawa Yipke au Sarpong aliyechangamka

    ReplyDelete
  10. Sawa,lkn Lwanga si wale Wabrazili /Wahindi mbona huwa hamuwataji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic