October 11, 2014


Yanga imeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Sekondari ya Loyola jijini Dar es Salaam huku ikionekana Kocha Marcio Maximo akipanga kuongeza kasi ya kikosi chake.

Yanga ni moja ya timu zinazocheza kwa kasi zaidi inapokuwa inashambulia.
Lakini inaonekana Maximo amepanga kuongeza kasi hiyo kabla ya pambano dhidi ya watani wake Simba, katika mechi itakayopigwa Jumamosi ijayo.
Kila wachezaji walipokuwa wakivuka eneo lao na kuingia kwenye upande wa wapinzani, aliwahimiza kucheza kwa kasi na pasi za haraka.
Hata hivyo, kocha huyo mara nyingi amelazimika kucheza mechi za kirafiki kwa kukigawa kikosi chake akidai anaathirika kutokana na kuwakosa wachezaji wake walio katika kikosi cha Taifa Stars kinachoivaa Benin, leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic