September 8, 2018


Timu ya Yanga kesho inashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon bila ya uwepo wa nyota wake watatu.

Yanga inakipima kikosi chake kwenye Uwanja wa Taifa majira ya jioni kuwaweka fiti wachezaji wake kuelekea mechi zijazo za ligi kuu.

Kuelekea mechi hiyo, Yanga itawakosa wachezaji Juma Abdul, Abdallah Shaibu na Juma Mahadhi ambao bado ni majeruhi.

Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema bado wachezaji hao wahajawa sawa kiafya hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi kesho.

Tayari viingilio vya mechi hiyo vimeshatajwa ambapo mzunguko utakuwa ni 3000, 5000 kwa VIP B na 10,000 kwa VIPA A huku watoto ni 1000.

1 COMMENTS:

  1. Wapuuzi nyie hivi Jana Simba haijacheza?FAKE NEWS

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic