September 7, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga leo utaweka hadharani sakata linalomkabili kiungo wao mpya Mohammed Issa Banka, aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar.

Yanga wameamua kuitisha kikao na waandishi wa habari ili kuliweka sawa suala la mchezaji wao ambaye imeripotiwa kuwa amefungikwa kwa miaka miwili na Shirikisho la Soka Africa (CAF) kutokana na matumizi ya sigara bwege 'Bangi'.

Baada ya taarifa hizo kutoka Yanga walikuja na kauli wakieleza kuwa wao hawana mamlaka ya kuliongelea huku wakisema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndiyo lina taarifa zake.

Inawezekana Yanga watakuwa walishakutana na TFF, hivyo tusubirie kikao hicho kitakuwa na yapi ya kuzungumzia kuhusiana na mchezaji huyo ambaye yupo kifungoni mpaka sasa.

Kiungo huyo inaelezwa kwa sasa yupo kwao Zanzibar akijifua mchangani ili kulinda kiwango chake mpaka pale kifungo alichopwa kitakapomalizika.

4 COMMENTS:

  1. KWANINI HUYU MCHEZAJI ASIJIFUE AKIWA YANGA MAZOEZINI WAKATI AKITUMIKIA KIFUNGO CHAKE? KWANINI YANGA IMEMNUNUA NA SASA HATA MAZOEZINI HAWEZI KUSHIRIKI ? KOSA LA YANGA LIKO WAPI HATA KUTOWEZA KUMTUMIA MCHEZAJI KWENYE MAZOEZI ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yupo sobber house midenda inamchuruzika kwa alosto aliyonaye,mchezaji wa hivyo atawezaje kufanya mazoezi wakati hata kusimama hawezi?

      Delete
    2. we unaongea nini!!!!,kauli yako mbona haiendani na habari yenyewe?.......hili ndo tatizo la mitandao,unaweza ukashangazwa na kubishana na mtu kwa kauli zake zisizo na kichwa wala miguu,kumbe wakati wewe umri wako ni mkubwa na IQ yako ni ya chuo kikuu mwenzako ana umri wa balehe au chini ya hapo na IQ yake ni ya darasa la tano.......unategemea nini hapo kama sio mambo yanayofanana ha hili.

      Delete
    3. Yawezekana hujuwi hata maana ya Hisa ya akili(intelligent quotient)na hata formular ya kukokotoa hisa ya akili huijuwi,nani aliyekuambia hisa ya akili inapimwa kwa kigezo cha madarasa uliyosoma?Ficha upumbavu wako.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic