October 24, 2018


Uongozi wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni kuhakikisha wanaendelea kupata matokeo mazuri ligi kuu ambapo kesho watacheza na KMC, suala la usajili litafuata baadaye.

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Novemba 15 kwa klabu zote zinazoshiriki ligi kuu kusajili wachezaji ambao wanawahitaji kuongeza nguvu ndani ya timu.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema kuwa wana mipango madhubuti ya kuboresha kikosi katika usajili huo, jukumu hilo wamemuachia kocha Mwinyi Zahera.  

“Tuna mipango ya kuboresha kikosi chetu kwenye usajili wa dirisha dogo, lakini kwa sasa muda bado haujafika hivyo tunasubiria hadi dirisha litakapofunguliwa ndio tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuzungumzia suala hilo.

“Muda ukifika ndio tutajua kina nani tutawasajili na wakinanani tutaachana nao kupitia kwa kocha ambaye ndiye atakayetoa mapendekezo juu ya suala hilo,"alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic