October 2, 2018


Imeelezwa kuwa kiungo wa klabu ya Yanga, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto amesema kung'ara kwa Simba juzi Taifa dhidi yao ni kutokana na mbinu alizotumia kocha wao.

Toto amesema kuwa Simba walikuwa wazuri zaidi haswa kwenye nafasi ya kiungo baada ya Kocha wao, Mwinyi Zahera kuwataka wasicheze kwa kushambulia.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka JKU ya Zanzibar amefunguka kuwa Zahera aliwapa mbinu ya kucheza huku wakijilinda ili kuepusha kuwapa nafasi ya upenyo wapinzani wao.

Safu hiyo ya kiungo iliyokuwa ikiongozwa na Jonas Mkude, Mgahana James Kotei na Mzambia Clatous Chama ilikuwa chachu ya Simba kuweza kuwashambulia zaidi Yanga.

Katika mechi hiyo, Simba na Yanga zilimaliza mchezo kwa matokeo ya bila kufungana (0-0).

11 COMMENTS:

  1. Mwanangu Fei endelea kujifunza kwani bado una safari ndefu hakuna anaekulaumu kwa kuzidiwa kiwango na machine za Simba kwenye gemu ya Jana. Yule kotei kafunga safari kutoka Ghana na tayari alshazunguka nchi kadhaa kabla kutua Simba ni beki mahiri wa kati yule ni namba mbili pia. Ni kiungo wa kati vile vile. Yule Mzambia Chama ni kiungo wa chipolopolo timu ya Taifa ya Zambia ni fundi yule.Mara ya mwisho mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia kuja kufanya kazi Tanzania ni zamani kweli kwa bahati nzuri unatoka Zanzibar wazee wa Malindi watakujuvya wakati wa akina Kenneth Malitoli Malindi ya Naushadi wakati huo. Ukija kwa mzawa Mkude ni miongoni mwa wachezaji wachache wazawa pale Simba wenye uhakika wa namba mbele ya mzungu. Kwa hivyo hakuna atakaekulaumu ulijitahidi sana ila ulizidiwa.

    ReplyDelete
  2. Kijana acha maneno ulizidiwa na hata ufanye nn bado huwezi shindana na majembe ya simba,ni huo u ccm tu ndio unaokufanya uitwe huko timu ya Taifa lakini kiwango chako bado sana.

    ReplyDelete
  3. Kijana acha maneno ulizidiwa na hata ufanye nn bado huwezi shindana na majembe ya simba,ni huo u ccm tu ndio unaokufanya uitwe huko timu ya Taifa lakini kiwango chako bado sana.

    ReplyDelete
  4. Huyo beans mdogo ana safari ndefu sana ili afike angalau nusu ya kiwango cha mwamba wa Lusaka, tripple C, moja ya viungo bora kabisa kuwai kutokea ktk taifa la zambia. Na bado Ana miaka mwili zaidi kukaribia kiwango cha mkude, kiungo bora kabisa Africa mashariki.

    ReplyDelete
  5. ni tanzania peke yake mchezaji anaonekana kuzidiwa lakini bado tu hakubali kwamba game ilikuwa ngumu kwa upande wake.... kinachosikitisha kuanzia kocha, wacheaji mpaka mashabiki wa yanga baada ya kuongea ukweli harithi kwqma game kwa upande wao ilikuwa ngumu na walizidiwa kila mbinu lakimi kocha anakwambia ile style nsiyo aliyowafundisha wachezaji wake wacheze, mchezaji anakwambia chama, mkude na kagere ni wachezaji wa kawaida sana hawana madhara, mashabiki wanakwambia ile kechi walikuwa ugenini hiv

    ReplyDelete
  6. mpira hauchezwi mdomoni walikuja wakina shishibaby wakasifiwa siku na simba wakaonekana hamna kitu simba ndiyo timu bora kwa viungo na kama angekuwepo Dilunga sijui ungesemaje mwishowe wangekutuhumu umenunuliwa

    ReplyDelete
  7. Fri Toto huna hadhi ya kujilinganisha Chama.Chama ni kiungo wa Chipolopolo ambao wameshawahi kuwa bingwa wa Afrika.Kuitwa kwenye timu hiyo sio mchezo.Jifunze wacha visingizio na ngebe.Kocha wenu amekiri kwamba uwezo mdogo ndio maana mlipaki basi. Hiyo ndio mbinu wanayotumia makocha wakiona timu yao upp dhaifu kuliko wapinzani wao.

    ReplyDelete
  8. Naona mashabiki wa simba mnajitoa ufahamu, kila mtu kiungo bora kiungo bora, msingekuwa na point 11 game sita kama mnakiungo bora, mpira ni matokeo chanya hayo mengine mbwembwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. usitoe ufaham ligi bado mbichi bado michezo zaidi ya 32, ubingwa upo wazi simba na usishangae hiyo yanga ishike nafasi hats ya tatu kushuka chin baada ya ligi kuisha

      Delete
    2. Manara kawaambia wao ndio timu bora na kwa vile ni mbumbumbu hawajiulizi mara mbili.
      Dogo hajashindana na viungo wa simba katoa maelekezo waliyopewa na kocha wakenashangaa hawa mbumbumbu wanamlisha maneno.

      Delete
  9. Kabisa unapomzungumzia Simba wa Tanzania basi unazungumzia viungo wa timu ya Taifa ya Tanzania ni utamaduni wa Simba miaka nenda rudi yakuwa na mahaba na wachezaji mahiri wa viungo toka zamani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic