October 2, 2018


Mlinda Mlango wa zamani wa klabu ya Simba, Mohammed Mwameja, amemsifia kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kutokana na mchango wake ndani ya Yanga.

Sifa hizo zimetoka mara baada ya Kakolanya kuonesha kiwango kikubwa katika mchezo dhidi ya Simba uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Radio One, Mwameja amesema kuwa mwanzo huo ni mzuri kwa Kakolanya na anapaswa kuzidi kupambana kwa kuwa ni tegemeo la baadaye kwenye timu ya Taifa Stars.

Aidha, Mwameja amemshauri Kakolanya kutokubweteka na badala yake anapaswa kuendelea kuonesha ukomavu zaidi ili kuhakikisha anaendelea kulinda kiwango chake.

"Alifanya vizuri kwakweli, nadhani anapaswa kuendelea kujituma zaidi ili kufika mbele zaidi ya hapo na asibweteke kwa namna alivyocheza dhidi ya Simba pekee. Ni mchezaji ambaye anaweza kuwa tegemeo wa Stars hapo baadaye" alisema Mwameja.

2 COMMENTS:

  1. Laiti ingekuwa sio ujasiri kipa huyo wa yanga, timu hiyo ingelifungwa si chini ya mabao matatu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa maana ingine pia unaweza sema kutokuwa makini kwa washambuliaji wa simba kumewakosesha bao si chini ya tatu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic